Kiswahili Teachers Workshop: Mang’u High School
MINT: KONGAMANO LA KITAIFA LA WALIMU WA KISWAHILI WA SHULE ZA UPILI
Idara ya Kiswahili ya Shule ya Upili ya Mang’u ikishirikiana na jumba la uchapishaji la Moran wana fahari kuu kuwaalika walimu wapendwa wa lugha ya Kiswahili wa shule yako kuhudhuria kongamano la kitaifa la kila mwaka.
Kongamano hili litafanyika katika ukumbi wa shule ya Mang’u siku ya Jumamosi tarehe 11 Mei, 2024 kuanzia saa mbili asubuhi.
Masuala yatakayoshughulikiwa
- Maelezo ya kina kuhusu riwaya ya Nguu za Jadi kutoka kwa mwandishi.
- Masuala ibuka katika utahini wa karatasi ya kwanza, pili na ya tatu.
- Maandalizi ya watahiniwa kwa ajili ya mitihani ya kitaifa ya Kiswahili.
- Mbinu bora za kufundisha vitabu vya fasihi (Nguu za Jadi, Bembea ya Maisha na Mapambazuko ya Machweo na Hadithi Nyingine).
Wawasilishaji waalikwa wa kongamano ni: - Prof. Clara Momanyi – Mwandishi, Nguu za Jadi
- Patrick Mandila
- Chite Rodgers
For More Updates Join Our WhatsApp Channel
Kila mwalimu mshiriki anatarajiwa kulipa shilingi elfu mbili na mia tano (Ksh. 2500). Uje na matini teule (Nguu za Jadi, Bembea ya Maisha na Mapambazuko ya Machweo na Hadithi Nyingine).
Thibitisha kushiriki kwako/kwenu kabla ya siku ya kongamano kwa minajili ya maandalizi kupitia kwa nambari yoyote ya rununu, kati ya zifuatazo: 0722800872/ 0720410677/ 0708292677.
Wako Mwaminifu,
Bi. Wachira-Mwandalizi
Mkuu wa Idara za Lugha
Nakala kwa:
Mkurugenzi wa elimu, Gatuzi Dogo la Juja Mkurugenzi wa TSC, Gatuzi Dogo la Juja
Mwenyekiti wa KESSHA, Gatuzi Dogo la Juja
FOR SUB-COUNTY DIRECTOR OF EDUCATION
PO BOX 753-01001 JUJA
In Our Other News: Mathematics Conference/Workshop: Asumbi Girls High School
Kiswahili Teachers Workshop: Mang’u High School